1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini

24 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E5S1

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu Johannesberg hii leo kupinga ghasia za chuki dhidi ya wageni zinazoendelea nchini Afrika Kusini.Waandamaji waliandamana huku wakibeba mabango yaliyoandikwa chuki dhidi ya wageni ni jambo linaloumiza kama ubaguzi wa rangi.Maandamano hayo yamepagwa na vyama vya wafanyikazi pamoja na makanisa nchini humo.Kiasi cha watu 50 wameuwawa katika vurugu za Afrika Kusini huku maduka yakitiwa moto pamoja na kuvunjwa.Rais Thabo Mbeki amewataka waafrika Kusini kutowatupa mkono waafrika wenzao na kuahidi kwamba serikali yake imejitolea kumaliza ghasia hizo.

Mashirika ya misaada yameonya kwamba wimbi linaloendelea la mashmbulio ya chuki dhidi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini

llinayaweka hatarini maisha ya maelfu ya wakimbizi kufuatia kitisho cha kuzuka kwa maradhi.Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema linawahudimia zaidi ya watu elfu 25 walioachwa bila maakazi.Shirika la madaktari wasiojali mipaka limesema kuwa watu huenda wakaambukizwa maradhi kutokana na kujaa kupita kiasi makambi ya wakimbizi.Maelfu ya watu wanakimbilia kambi hizo kutokana na kuenea ghasia hizo ambazo zimeingia hadi Cape Town mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.