1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macky Sall ashinda nchini Senegal

Abdu Said Mtullya26 Machi 2012

Kiongozi wa upinzani Macky Sall ameshinda katika raundi ya pili ya uchagauzi wa Rais nchini Senegal. Maalfu ya watu wamejitokeza katika mitaa ya mji Mkuu Dakar kusherehekea ushindi wa Sall

https://p.dw.com/p/14S47
Macky Sall mshindi wa uchaguzi wa urais nchni Senegal
Macky Sall mshindi wa uchagauzi wa urais nchini SenegalPicha: AP

Katika uchaguzi wa Rais nchini Senegal Rais Abdoulaye Wade amekubali kushindwa.

Televisheni ya serikali imearifu kwamba Rais huyo mwenye umri wa miaka 85 alimpigia simu kiongoziwa upinzani Macky Sall na kumpongeza kwa ushindi, baada ya matokeo ya awali kuonyesha kwamba Sall ameshinda kwa kura 30,000 wakati Wade amepata kura 11,000

Maalfu ya watu wamesherehekea ushindi wa Macky Sall katika mitaa ya mjini Dakar mapema asubuhi.
Watu hao walianza kusherehekea hata kabla ya Rais Wade kukubali kushindwa.Vyombo vya habari vya serikali nchini Senegal vimeshaanza kutoa mfululizo wa matokeo ya uchaguzi uliofanyika hapo jana.

Hofu kwamba Rais Wade angelijaribu kung'ang'ania madaraka au kuyapinga matokeo ya uchaguzi ilisababisha mapambano mabaya katika siku za kuelekea kwenye uchaguzi. Wanaharakati wa upinzani walisema hatua ya Wade ya kugombea muhula wa tatu wa Urais ilikuwa kinyume na katiba.Matokeo rasmi ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa mnamo kipindi cha saa 48.

Mwandishi:Mtullya Abdu/AFP,AP,Reuters

Mhariri: A.Schmidt