1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Macron arefusha ziara yake kisiwani Mayotte

20 Desemba 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amerefusha leo ziara yake katika kisiwa cha Mayotte kilichoharibiwa na kimbunga Chido.

https://p.dw.com/p/4oPS9
Macron | Chido | Mayotte
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza na wenyeji alipowasili Hospitali ya Mayotte mjini Mamoudzou kufuatia kimbunga Chido kupiga kisiwa hicho.Picha: Marin Ludovic/abaca/picture alliance

Hii ni baada ya wakaazi waliojawa na ghadhabu kuelezea kero zao na hali ya kukata tamaa kutokana na ukubwa wa maafa hayo.

Wenyeji walimzoea Macron na kutoa malalamiko yao jana wakati alikitembelea kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi, siku tano baada ya kimbunga Chido kusababisha uharibifu mkubwa.

"Kwanza kabisa nataka kuwaambieni kuwa najua mmekuwa na wakati mgumu katika siku sita zilizopita. Hofu kutokana na hiki kimbunga. Sikuhusika kwa vyovyote na kimbunga hicho. Mnaweza kunilaumu, lakini haikuwa mimi.

Timu za uokozi zinaendelea kuwatafuta manusura na kugawa msaada unaohitajika kwa dharura. Idadi ya awali iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa inaonyesha kuwa watu 31 wamethibitishwa kufa na 2,500 kujeruhiwa.

Kimbunga Chido kimewauwa kiasi ya watu 73 nchini Msumbiji.