Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ina utajiri wa aina mbalimbali za madini, na makampuni mengi ya kigeni huwania utajiri huo, huku mashirika ya haki za binaadamu yakiangazia wanaofanyishwa kazi hiyo ngumu ya uchimbaji na kutofaidika chochote, hususan watoto na vijana. Mohammed Abdulrahman atakufahamisha zaidi changamoto zinazokabili kada hizo kwenye machimbo ya madini ya Colbat huko Katanga.