1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watoto wa Ukraine wamepelekwa Belarus

17 Novemba 2023

Zaidi ya watoto 2,400 kutoka Ukraine walio na umri wa kati ya miaka sita hadi 17 wamepelekwa nchini Belarus tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Z3YO
Ujerumani, Berlin |Wakimbizi wa Ukraine
Wakimbizi wa UkrainePicha: Michael Kuenne/PRESSCOV/ZUMA/picture alliance

Ni kulingana na ripoti ya uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Yale na kuchapishwa Alhamisi. Ripoti hiyo imeeleza kuwa watoto hao wamepelekwa katika vituo 13 kote Belarus.

Mnamo mwezi Mei, mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine alisema alikuwa anachunguza madai ya kuhusika kwa Belarus katika kashfa ya kuwahamisha kwa lazima zaidi ya watoto 19,000 kutoka maeneo yanayokaliwa na Urusi tangu mzozo wao ulipoanza.

Matokeo ya uchunguzi huo wa chuo cha Yale ndiyo ya kina zaidi hadi sasa kuhusu tuhuma dhidi ya Belarusi katika mpango wa uhamishaji wa Urusi kwa watoto wa Ukraine.

Awali Urusi ilijitetea kuwa inatoa misaada ya kibinadamu kwa wale wanaotaka kukimbia Ukraine kwa hiari na ilikataa tuhuma za uhalifu wa kivita dhidi yake.