JamiiRwanda
Mafuriko makubwa yamewaua watu 129 nchini Rwanda
4 Mei 2023Matangazo
Kulingana na ripoti ya shirika la utangazaji habari la Rwanda, idadi ya vifo inazidi kuongezeka.
Mvua kubwa ilianza kunyesha wiki iliyopita na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba kadhaa kote nchini na kuharibu baadhi ya barabara.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Rwanda imetahadharisha kwamba mvua nyingi bado zinatarajiwa.
Baadhi ya nchi za kanda ya Afrika Mashariki ikiwemo kusini magharibi mwa Uganda, pia zinakumbwa na mvua kubwa.
Wiki iliyopita, watu wasiopungua watatu walikufa maji baada ya kusombwa na mafuriko katika Kijiji cha Rukungiri Uganda.