Matangazo
Lakini mageuzi hayo yatachukuwa muda kabla ya kufikia malengo yake ambayo ni kujitegemea kifedha kwa Umoja wa Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa wa Tanzania, Dokta Augustine Mahiga ambae ameongoza ujumbe wa nchi yake mjini Addis Ababa, Ethiopia ameelezea masuala muhimu yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho ikiwemo ufumbuzi wa mizozo ya kikanda.
Kwenye mahojiano ya kipekee na mwandishi wetu Saleh Mwananamilongo, Balozi Mahiga ameanza kwanza kuelezea agenda ya mkutano huo.