Mjini Kinshasa, wafuasi wa mwanasiasa na kiongozi wa kidini Nemwanda Nsemi wamekabiliana na polisi wakati walipokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea Ikulu, katika jaribio la kumuondoa madarakani rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi. Mwandisi wetu wa mjini Kinshasa Jean- Noel Bamweze alizungumza na Sylvia Mwehozi ili kufahamu hali ilivyo kwa hivi sasa mjini Kati.