Asili na mazingiraKorea Kusini
Makubaliano kuhusu taka za plastiki yashindwa kupatikana
2 Desemba 2024Matangazo
Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa juhudi za kukabiliana na uchafuzi unaoongezeka wa mazingira utokanao na taka za plastiki.
Suala kuu lililoleta utata ni uwezekano wa kuweka kiwango cha uzalishaji wa plastiki, kama ilivyotakiwa na muungano wa mataifa zaidi ya 100 yaliyokuwa na mtazamo sawa, yakiwemo Mexico, Panama, Rwanda na Umoja wa Ulaya.
Lakini mataifa yanayochimba mafuta kama Saudi Arabia na Urusi yamepinga vikali hatua hiyo na badala yake yakataka makubaliano hayo yajikite katika njia bora za kutupa taka za plastiki.
Duru hii ya tano ilichukuliwa kuwa ya mwisho ya mazungumzo hayo, lakini sasa mjadala huo utaendelea mwakani.