1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini kwa Vijana wa Iran

18 Januari 2016

Makubaliano ya mradi wa nyuklia wa Iran, na mvutano kuhusu wakimbizi ndizo mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1HfEC
Kiwanda cha Mafuta cha IranPicha: picture alliance/AP Photo/V. Salemi

Tunaanza na matumaini ya kibiashara yaliyozuka baada ya kuanza kufanya kazi makubaliano ya kimataifa kuhusu mradi wa nyuklea wa Iran. Gazeti la "Flensburger Tageblatt" linaandika:"Wajerumani hawabidi kushangiria mapema. Kuna mengi ya yanayokorofisha soko doro la Iran kuanza upya kunawiri. Mojawapo ni soko dhaifu la mafuta ambalo haakuna anaetegemea kwa kurejea Teheran litaimarika . Kuna hofu zisizokwisha pia za Israel na Mmarekani. Na pia mzozo unaozidi makali kati ya Saud Arabia na Iran. Hakuna yeyote anaeweza kuhakikisha kama mmojawapo wa mahasimu hao hatoitaja Ujerumani ijizuwie kufanya biashara na adui-mfano katika biashara ya silaha.

Vijana wa iran wajiwekea matumaini

Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linahisi kuanza kufanya kazi makubaliano ya mradi wa nyuklia wa Iran ni fursa nzuri ya kuanza mageuzi nchini humo."Gazeti linasema asili mia 70 ya wakaazi milioni 78 wa Iran ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 30 na muasisi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Ayatollah Khomeini,hawamjui, wanasikia tu akitajwa. Makadirio ya kufunguliwa milango demokrasia ni makubwa katika nchi hiyo ya kiislamu kuliko katika nchi yyoyote ile nyengine ya Mashariki ya kati. Mashirika ya kiraia yameendelea zaidi kuliko yale ya nchi za kiarabu. Wananchi ni wasomi na wenye nidhamu. Vijana wa Iran wana kipaji kikubwa pia kuliko wenzao katika eneo hilo. Wanajua wanataka nini. Na wanaamini,wakati wao utafika haraka.

Ujerumani yahitaji soko huru na watu kutembelea barani Ulaya

Mjadala kuhusu wakimbizi unazidi kuhanikiza humu nchini.Gazeti la "Bild" linahisi siasa ya kansela Merkel ya kuwafungulia milango imelengwa pia kuunusuru Umoja wa Ulaya. Gazeti linaendelea kuandika:"Sweeden imeifunga mipaka yake. Hungary tangu zamani,Slovenia imezungusha senyenge kuzuwia wimbi la wakimbizi na kansela Merkel anaacha wazi mipaka ya Ujerumani. Anaachia mpaka wakimbizi kutoka nchi salama mfano wa Austria kuingia humu nchini. Kwasababu ya hofu,Ulaya pengine inaweza kuvunjika,pindi akiregeza kamba. Ndo kusema Ulaya kwake ni muhimu zaidi kuliko Ujerumani? Nchi aliyoapa,alipokabidhiwa hatamu za uongozi,kuiepushia balaa?Merkel anaifikiria Ujerumani kabla ya Ulaya. Kwakua Ujerumani ni nguvu kubwa ya kiuchumi, inahitaji uhuru wa watu kwenda wakutakako na bidhaa kuingia bila ya pingamizi katika nchi za Umoja wa ulaya. Hatari iliyoko ni kwamba pindi Merkel akiifunga mipaka,wote wengine watafanya hivyo hivyo. Hapo soko la pamoja,saraafu ya Euro na juhudi za amani itakuwa kazi bure. Na hapo Ujerumani pia itaathirika vibaya sana. Kwa kufuata mkondo huo,Angela Merkel anajaribu kwa hivyo kuiokoa Ulaya ambayo Ujerumani inaihitaji. Njia anayoifuata ni ya hatari,kwake yeye binafsi na kwa nchi yetu. Lakini kutojaribu ingekuwa hatari zaidi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman