MichezoGuinea
Makumi ya watu wafariki Guinea katika mkanyagano
2 Desemba 2024Matangazo
Watu 56 ambao walikuwa ni mashabiki wa soka wamekufa katika mkanyagano kusini mwa Guinea wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vikijaribu kutuliza vurugu wakati wa mechi ya soka kwenye uwanja uliokuwa umefurika watazamaji.
Mkanyagano huo ulitokea wakati watu walipojaribu kutoka uwanjani humo, huku wengi wao wakiruka uzio mrefu kuepuka vurugu hizo. Mechi hiyo iliyochezwa Jumapili mchana katika mji wa Nzerekore ilikuwa ni fainali kati ya timu za Labe na Nzerekore na ilikuwa ni kwa heshima ya kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Mamadi Doumbouya.
Waziri Mkuu wa Guinea Amadou Oury Bah amesema mamlaka zinaendelea na hatua za kurejesha utulivu katika eneo hilo.