1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Mali yadai kumkamata kiongozi wa IS kanda ya Sahel

17 Desemba 2024

Jeshi la Mali limedai kwamba limemkamata "kiongozi mkuu" wa tawi la kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu, IS, kwenye kanda ya Sahel.

https://p.dw.com/p/4oEAy
Mali | Usalama
Mali imekuwa inapambana na uasi wa wapiganaji wenye mafungamano na makundi mawili ya itikadi kali ya IS na Al-Qaeda.Picha: AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake iliyochapishwa jana, Jeshi la Mali limesema vikosi vyake kwenye mkoa wa mashariki wa Menaka "vimemkamata Ahmad Ag Ditta" iliyemtaja kuwa kiongozi wa tawi la kundi la IS kanda ya Sahel linalofahamika kwa kifupi kama EIGS.

Limedai kwamba Ditta "anahusika na uhalifu mkubwa dhidi ya raia wasio na hatia, na ndiye mratibu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo".

Jeshi pia limesema kwenye operesheni yake limefanikiwa kuwaua wapiganaiji wa EIGS na kukamata vifaa kadhaa vya kijeshi ikiwemo mabomu yanayoundwa kienyeji.

Mali, taifa la Afrika Magharibi, linakabiliwa na mzozo wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi na tangu mwaka 2012 linapambana na uasi wa wapiganaji wenye mafungamano na makundi mawili ya itikadi kali ya IS na Al-Qaeda.