JamiiCuba
Mamilioni ya watu hawana umeme Cuba
5 Desemba 2024Matangazo
Shirika kuu la kusambaza umeme la nchi hiyo limesema kwamba linaweza kusambaza megawati 533 tu za umeme kati ya megawati zaidi ya 3,000 zinazohitajika.
Mapema serikali ya nchi hiyo ilisema ingelitoa kipaumbele kwa mahospitali na vituo vya kusambaza maji. Skuli na huduma zisizo za lazima za serikali zimefungwa hadi hapo baadaye.
Soma zaidi: Mamilioni ya Wacuba gizani baada ya umeme kukatika nchi nzima
Mji mkuu, Havana, unaendelea kusalia kwenye giza, ingawa kampuni ya umeme kwenye mji huo imesema zaidi ya wateja 260,000 wamerejeshewa huduma hiyo.
Utoaji umeme katika taifa hilo la Karibiani unakaribia kushindwa kabisa, kutokana na uhaba wa mafuta, majanga ya kimaumbile na mzozo wa kiuchumi.