1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Baada ya Sudan Kusini kuunda serikali ya kitaifa.

Admin.WagnerD24 Februari 2020

Wajumbe maalumu katika usuluhishi wa mzozo wa Sudan Kusini wametoa mwito kwa watu nchini humo kuhakikisha wanailinda fursa waliyopata kwa kulijenga taifa lao baada ya kuundwa kwa serikali.

https://p.dw.com/p/3YHNp
Äthiopien Addis Abeba Südsudan Friedensverhandlungen
Picha: DW/G. Tedla

Baada ya rais Salva Kiir na mpinzani wake Dr Riek Machar kuunda serikali ya umoja wa kitaifa mwishoni mwa juma aliekua mjumbe maalum wa Kenya kwenye mazungumzo hayo Bw Kalonzo Musyoka na Prof Joram Biswaro wa Umoja wa Afrika wamewataka wa Sudan wasiipoteze tena fursa hii kwa mara ya pili ili kujenga taifa lao. 

Sudan Kusini ilifungua ukurasa mpya katika mchakato wake tete wa kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya viongozi hasimu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo waangalizi wengi wameomba idumu safari hii.

Siku moja baada ya rais Kiir kuvunja serikali ya awali kiongozi wa upinzani Riek Machar aliapishwa kama makamu wake, katika utaratibu ambao ulishindwa kutimiza lengo mara mbili. Ilikua ni shamra shamra vifijo na nderemo wakati Machar alivyoapishwa na kufuatiwa na makamu wa rais wengine wanne.

Baadae nilipata fursa ya kuzungumza na Bw Kalonzo Musyoka ambae mjumbe maalum wa Kenya kwenye mazungumzo. Nae Prof. Joram Biswaro mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Sudan Kusini alikua na furaha kupita kiasi.

Lt Gen mstaafu Augostino Njoroge amekua mweyekiti wa tume ambayo imekua ikifatilizia na kutathmini mazungumza haya Sudan Kusini amesema kazi sasa imekwisha yaliobakia wanawaachia wa Sudan Kusini wenyewe CLIP

Hapo jana makamu wa rais wa 5 Hussein Abdul Bagi kutoka chama cha SSOA muungano wa vyama vya upinzani ndipo alipo apishwa rasmi baada ya kumaliza ugomvi wao ndani ya chama hicho juu ya nani angelikua makamu wa rais.

Taifa hilo changa kabisaa lilitumbukia kwenye mgogoro wa vita vya wenywe kwa wenywewe mwaka 2013, miaka miwili baada ya kupata uhuru wake kutoka Sudan, kufuatia mapambano kati ya wafuasi wa Kiir na Machar.

Omar Mutasa DW Juba, Sudan Kusini