Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linasema idadi ya wakimbizi duniani ni kubwa zaidi kuliko raia wote wa Ufaransa na Uingereza wakichanganywa pamoja, ambapo hadi mwishoni mwa 2017, watu milioni 68.5 walijikuta ukimbizini, likiwa ni ongezeko la watu milioni 3 ikilinganishwa na 2016, lakini wanaoikimbilia Ulaya inashuka. Kwa nini? Mohammed Khelef anaongoza Meza ya Duara.