Hali imekuwa ya wasiwasi mkubwa asubuhi ya leo kwenye mji wa Kalengera na mingine kadhaa midogo katika wilayani ya Rutshuru mashariki mwa Kongo, ambako mapigano makali yalishuhudiwa kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23. Duru zinasema shughuli za usafiri zilikatizwa kwenye barabara kuu kutoka Goma kuelekea kwenye mji mkuu wa wilaya hiyo ya Rutshuru. Msikilize Benjamin Kasembe.