Duru za mashirika ya misaada katika mkoa wa Ituri ulio Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema watu zaidi ya Laki mbili wa mkoa huo wameyakimbia makazi yao, kutokana na vurugu za kikabila. Daniel Gakuba amezungumza na Jean Bosco Lalo, mkuu wa mashirika ya kiraia katika mji wa Bunia, ambaye amekanusha taarifa kuwa mapigano hayo ni ya kikabila.