Mapinduzi ya vyombo vya habari yanahitajika Zimbabwe
29 Aprili 2013Vitisho hivyo vinatajwa kutoka chama tawala cha Zanu-PF ikiwa changamoto katika kueleka mageuzi ya vyombo vya habari kufatia makubaliono ya kisiasa yalio fikiwa mwaka 2008 kati ya chama cha Zanu-PF na chama cha vuguvugu la mabadiliko ya kidemokrasia ambayo yalifungua njia ya kuunda serikali ya sasa ya umoja wa kitaiafa na kuandaa uchguzi ujao mwaka huu.
Makubaliano hayo yanaitaka ,serikali ya Zimbabwe kufanya magaeuzi katika sekta ya ulinzi na vyombo vya habari, ili ifanikiwe kufanya uchaguzi wa huru na haki mwaka huu,pamoja na kufanya mabadiliko katika tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo inatajwa kuwa na wafanyakazi wengi wa usalama wa taifa.
Mbali na hayo serikali ya Zimbabwe inahitaji kufanya marekebisho katika sheria zake, kama sheria ya haki ya kupata habari na kulindwa wanahichi ambayo inasema kuwa wanadishi wa habari wanatakiwa kusajiliwa kila mwaka katika Baraza la vyombo vya habari nchini humo.
Charles Hungwe wa mahakama ya kuu nchini humo anatuhumiwa na chama tawala cha Zanu-PF kufuatia hatua yake kusaidia tume ya kupambana na Rushwa na kuiachia kufanya uchuguzi katika chama tawala,wanasiasa wanaodaiwa kuhusika katika Rushwa na kudhamini ulinzi kwa mwanasheria maarufu nchini humo Beatrice Mtetwa.
Beatrice Mtetwa anatuhumiwa kwa kutoa madai ya kufanyika uadilifu kwa kuomba jeshi la polisi nchini humo kuonesha hati ya mashtaka wakati walipovamia ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Morgan Tsvangirai mapema Machi mwaka huu.
Mchambuzi wa mambo ya kisisa Rejoice Ngwenya amesema kama hakutafanyika mageuzi katika vyombo vya habari,wandishi wa habari watakuwa na wakati mgumu na maafisa wa usalama wa taiafa hilo, kutokana na sheria kuwabana wandishi kufanya kazi zao.
Amesema lazima yafanyike mageuzi katika vyombo vya habari kama sehemu ya makubaliano ya GPA, licha ya kuwa chama tawala cha Zanu-PF kikipinga jambo hilo ambalo katiba mpya ya Zimbabwe inataka mageuzi hayo yafanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kukandamiza vyombo vya habari
Magazeti ya The Daily News,NewsDay na Zimbabwe Independent,ambayo yanamilikiwa na watu binafs,anameshitakiwa na wanasia kwa kuchapisha habari za,madai ambayo wachambuzi wa kisiasa wanadai kuwa ni kutaka kunyamanzisha vyombo vya habari, katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mkurugenzi wa kampuni ya Media Center nchini Zimbabwe Ernst Mudzengi,amesmeas kuwa imekuwa jambo la kawaida kwa wandishi wa habari nchini Zimbabwe kukabiliwa na vitisho na changamoto zingine hasa wakati wa uchaguzi.
Chama cha wandishi wa habari Zibambwe ZUJ kimsema kuwa kuwa vitisho dhidi ya wandishi wa ahabri vinazidi kila siku wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mkuu Juni 29 mwaka huu.
Madai hayo yamepingwa na But Bright Matonga mchambuzi wa shirika la utangazaji la Zimbabwe na kusema kuwa kuna mazingira mazuri kwa vyombo vya habri, ingawa baadhi ya wandishi hawataki kuwajibika na ripoti zao, kinachotakiwa kwa sasa kwa wandishi hao ni kutii sheria hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Wachunguzi wa wa kimataifa wa haki za binadamu kutokaMarekani wanadai kuwa sheria zote hizo zimkuwa zikitumika na chama cha Zanu-PF kuwatisha na kuwatesa wanasisa na wanaharaki wa haki za binadamu,na kuzuia wanahabari kutoa lawama zao na kufanya mijiadala ya umma.
Mwandishi: Hashim Gulana
Mhariri: Mohammed Khelef