1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBenin

Marekani kusaidia Afrika Magharibi kudhibiti uasi

8 Aprili 2023

Marekani imesema inaandaa msaada wa muda mrefu kwa mataifa matatu ya Ivory Coast, Benin na Togo kufuatia kitisho cha kusambaa kwa uasi wa makundi ya itikadi kali kwenye mwambao wa Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4PptJ
Pwani ya Afrika Magharibi
Pwani ya Afrika Magharibi Picha: Alida Latham/Danita Delimont/Imago Images

Hayo yameripoti na shirika la habari la AFP likiwanukuu maafisa kadhaa wa serikali ya Marekani akiwemo naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani anayeshughulikia kanda ya Afrika Magaribi, Michael Heath.

Maafisa hao wamesema msaada wa mataifa ya magharibi ni muhimu kwenye kanda hiyo ili kudhibiti kusambaa kwa hujuma za makundi ya itikadi kali na ushawishi wa Urusi kupitia kundi la mammluki la Wagner.

Chini ya mpango unaojadiliwa, mataifa ya mwambao wa Afrika Magharibi yatanufaika kwa msaada wa kifedha kuimarisha uchumi, uwezo wa idara za usalama na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.