1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaikazia macho Pyongyang

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiR

Beijing. Marekani imeitaka Korea Kaskazini kutekeleza wito wa kuitaka iche mpango wake wa kutengeza silaha za nuklia.

Mjumbe wa Marekani wa ngazi ya juu Christophe alitoa wito mjini Beijing ambako alikowasili katika mazungumzo juu ya mpango huo wa Korea Kaskazini.

Amesema kuwa natarajia kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na mwakilishi wa Korea Kaskazini, Kim-Kye-Gwa, ambaye hapo siku ya Jumamosi aliilaumu Marekani kwa siasa zake za kiuhasama .

Christopher Hill amesema kuwa mazungumzo hayo yanelekea njia panda.

Mazungumzo hayo yanakuja miezi miwili baada ya Korea Kaskazini, kufanya majaribio yake ya kwanza ya kombora la nuklia.

Nchi sita zinazoshiriki katika mazungumzo hayo ya mjini Beijing, mbali na wenyeji China ni pamoja na Korea Kaskazini yenyewe, Korea Kusini, Marekani, Japan na Urusi.