SiasaHaiti
Marekani yalaani mauaji ya vikongwe 200 nchini Haiti
11 Desemba 2024Matangazo
Marekani imelaani vikali mauaji ya takriban watu 200 yaliyofanywa na wanachama wa genge moja la uhalifu nchini Haiti.
Msemaji wa ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre amesema ripoti ya kutokea mauaji hayo imeishtusha Marekani.
Siku ya Jumatatu ofisi ya waziri mkuu wa Haiti ilisema kwamba takriban watu 180 wengi vikongwe waliuwawa mwishoni mwa juma katika eneo la Cite Soleil baada ya kushambuliwa.
Shirika moja lisilokuwa la kiserikali lilisema kwamba mashambulio hayo yaliamrishwa na kiongozi wa genge moja la wahalifu ambaye anashuku mwanawe amepata maradhi baada ya kufanyiwa mambo ya kishirikina.