Mashambulizi ya Israel Gaza yaua watu 8 wa familia moja
17 Desemba 2024Matangazo
Shambulizi hilo lililofanyika siku ya Jumatatu usiku lililenga nyumba moja katikati mwa Gaza katika eneo jirani la Daraj. Miongoni mwa miili iliyopatikana na ya baba na wanawe watatu pamoja na bibi ya watoto hao. Israel bado haijatoa tamko lolote juu ya shambulizi hilo. Kulingana na wizara ya afaya ya Gaza, kwa ujumla mashambulizi ya Israel mjini humo yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 45,000 ndani ya miezi 14 na wengi wa waliouwawa ni wanawake na watoto. Israel ilianzisha awamu hii ya mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza kujibu mashambulizi ya kundi la Hamas kusini mwa Israel yaliyosababisha mauaji ya watu 1,200.