Mashambulizi ya Israel yauwa mtu 1 Lebanon
9 Desemba 2024Matangazo
Katika mashambulizi hayo, wanajeshi wanne wa Lebanon wamejeruhiwa huku makubaliano ya kusitisha vita ambayo ni hafifu yakiendelea kutekelezwa.
Jeshi la Israel katika taarifa yake limesema mashambulizi hayo yalitokea pale maadui walipolilenga gari moja karibu na kizuizi cha kijeshi cha Saf al-Hawa/Bint Jbeil.
Waziri wa Afya wa Lebanon, Firass Abiad, amesema mpaka sasa idadi ya watu waliouawa katika vita vya zaidi ya mwaka mmoja kati ya Israel na Hezbollah imefikia watu 4,047 wakiwemo watoto 316.