Mashambulizi ya Mumbai yamalizika
29 Novemba 2008Kuuwawa kwa mwanamgambo huyo kumemaliza mapambano ya siku tatu katika sehemu saba mashuhuri katika mji mkuu huo wa kibiashara nchini India ambayo yameuwa watu 195. Katika juhudi za mwisho za kuidhibiti hoteli hiyo wanamgambo watatu wa itikadi za Kiislam wameuwawa pamoja na komandoo mmoja wa India.Utafutaji wa mabomu yaliotegwa kwenye hoteli hiyo unaendelea.Awali makomandoo hao wa India waliwazidi nguvu wanamgambo hao katika hoteli nyengine ya kifahari ya Trident- Oberoi na kituo cha utamaduni cha Kiyahudi.Serikali ya India inasema watu 195 wamekufa kutokana na mashambulizi hayo wakiwemo raia wa kigeni 18 na watu wengine 295 wamejeruhiwa. Mashambulizi hayo ni aina yake kuwahi kutokea nchini India anasema Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh.
Serikali ya India inaamini kwamba washambuliaji hao waliingia katika mji huo wa harakati kubwa wa bandari kwa kutumia mashua ndogo.Kuna habari za kutatanisha juu ya wanamgambo waliohusika na mashambulizi hayo lakini mmojawao anashikiliwa na polisi.