1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya haki yataka mwanaharakati wa Niger aachiwe

10 Desemba 2024

Mashirika ya matatu ya haki za binaadamu yametoa wito kwa utawala wa kijeshi Niger kumuwachia huru mwanaharakati wa muda mrefu wa asasi za kiraia anayeshikiliwa kizuizini.

https://p.dw.com/p/4nwzN
Mwanaharakati wa Niger,  Moussa Tchangari
Mwanaharakati wa Niger, Moussa Tchangari.Picha: António Cascais/DW

Mashirika hayo yanazituhumu mamlaka kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza na upinzani wa kisiasa. Moussa Tchangari, mkosoaji wa watala wa kijeshi ambaye awali alielezea uungaji mkono kamili wa rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum, alikamatwa na watu wasiojilikana waliokuwa na silaha nyumbani kwake katika mji mkuu Niamey Jumanne wiki iliyopita.

Mashirika ya Amnesty International, Human Rights Watch na Observatory for the Protection of Human Rights Defenders yamesema Tchangari alikamatwa kwa sababu ya kutekeleza kwa amani haki zake za kibinaadamu.

Mashirika hayo matatu yalihusisha kukamatwa huko na kile yalichokisema ni ukandamizaji uliokithiri wa mamlaka za Niger dhidi ya upinzani wa kisiasa, vyombo vya habari na ukosoaji tangu Jenerali Abdourahamane Tiani alipotwaa madaraka Julai mwaka jana.