Miongoni mwa tuliyo nayo asubuhi ya leo: Leo ni miaka 45 tangu alipouwawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume. Mchakato wa uteuzi wa wagombea nchini Kenya ndani ya vyama unatishia kuvipasua vyama vyote. Na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, leo inasikiliza kesi ya kwa nini Afrika ya Kusini ilishindwa kumkamata Rais Omar Al Bashir wa Sudan wakati wa ziara yake ya mwaka 2015.