Miongoni mwa mengi tuliyokuandalia asubuhii hii ni pamoja na matokeo ya kuahirishwa uchaguzi wa Jumapili huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ameamua kuondoka kwenye utawala wa Trump. Na wasanii nchini Kenya wameanzisha harakati za kuufufua utamaduni wa kutamba hadithi kutumia njia za kisasa.