Miongoni mwa utakayoyasikia kwenye matangazo haya: Raia wa Gabon leo Agosti 26 wanapiga kura katika uchaguzi wa Rais, bunge na serikali za mitaa. Rais aliye madarakani, Ali Bongo anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo unaoweza kumuweka madarakani kwa muhula wa tatu. Ameitawala nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta tangu aliposhinda uchaguzi baada ya kifo cha baba yake Omar Bongo mwaka 2009.