Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ametoa wito kufikiriwa upya mtazamo wa nchi yake kuelekea Uturuki // Rais Donald Trump wa Marekani ameliomba baraza la Congress kumpatia dola bilioni 7.85 ili kukabiliana na maafa ya kimbunga Harvey // Mamia ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, wamehamishiwa kwenye mpaka wa Iraq.