Mazungumzo kutatua mkwamo katika shughuli za serikali ya Marekani yataendelea leo. Maafisa wa Ujerumani walaumiwa kwamba walikuwa na taarifa kuhusu udukuzi wa data za wanasiasa akiwamo kansela Angela Merkel. Na, jumuiya ya kimataifa yaionya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuheshimu matokeo ya uchaguzi yakiwa bado yanangojwa kutangazwa.