Rais wa Marekani Donald Trump asema siku zijazo zitakuwa "mtihani halisi" katika kupona kwake COVID-19, Ufaransa yarekodi maambukizi mapya ya juu ya virusi vya corona ya takriban 17, 000 na ongezeko la vifo 49 ndani ya siku moja na maafisa katika eneo la Nagorno-Karabakh wasema maeneo ya raia katika mji mkuu wa eneo hilo yameshambuliwa kwa makombora yaliyorushwa na jeshi la Azerbaijani.