Ethiopia na Eritrea zilisaini makubaliano katika mkutano wa kilele uliofanyika Saudi Arabia, hivyo kuimarisha mkataba wa amani kati ya mahasimu hao wawili wa zamani katika pembe ya Afrika. Mfalme Salman wa Saudi Arabia alikuwa mwenyeji wa hafla hiyo. Jiunge na Josephat Charo akiwa na Maimuna Mwidau, Anaclet Rwegayura na Profesa David Monda katika kipindi cha Maoni.