Wakaazi wa mji wa Beni ulio mashariki mwa Kongo, Beni, wameungana na wenzao kutoka Butembo kuandamana tangu asubuhi, kufuatia mauwaji ya raia wanane usiku wa kuamkia leo (Novemba 25) yaliyofanywa na waasi. Huku wakiwa na hasira, waandamanaji hao baada ya kuchoma moto ofisi ya meya wameelekea kwenye kambi ya MONUSCO ambako muandamanaji mmoja aliuawa. Sikiliza ripoti ya John Kanyunyu.