Mauaji ya Kasai, DRC yachunguzwe
2 Juni 2017Imekuwa vigumu kwa wanaharakati wanaopigania haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linafuatilia vurugu hizo, kufikia eneo hilo, kwa hiyo idadi hasa, ya watu waliouwawa inaweza kuwa zaidi ya hao.
"Vurugu katika sehemu ya Kasai limewafanya watu wateseke sana, mamlaka ya Congo imeshindwa au haitaki kuwashutumu wanaohusika kwa unyaunyasaji wanaofanya," alisema Ida Sawyer ambaye ni mkuu wa Afrika ya kati wa shirika linalotetea haki za binadamu la Human Rights Watch.
Mkuu huyo pia alisema kuwa uchunguzi huru wa kimataifa unahitajika kufanyika, kufuatilia unyanyasaji huo na lazima kuwatambua wahusika ili haki itendeke kwa waathirika.
Jeshi la Congo limetumia nguvu kwa wale wanaovunja sheria za kimataifa, kuwauwa wanaofikiriwa kuwa wanachama wa kundi la KAMUINA NSAPU wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Wanachama wa kundi hilo, mara nyingi hutumia magongo na silaha wanazotengeneza wenyewe, kundi hilo pia huwatumia watoto katika mapambano yao na hufanya mashambulizi katika sehemu za serikali, huwauwa maafisa, askari na maafisa wa ndani.
Wataalamu wawili kwa ajili ya eneo la Congo wa Umoja wa Mataifa, Zaida Catalan, kutoka Sweden na Chile na Michael J. Sharp kutoka Marekani waliuliwa Machi 2017, wakati walipokuwa wakifanya uchunguzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo. Mpaka sasa haijulikani nani anahusika na mauaji hayo, na wakongo wanne ambao walifuatana nao mkalimani: Betu Tshintela na waendeshaji pikipiki watatu bado hawajulikani walipo.
Wachunguzi wa Umoja wa mataifa wamethibitisha kuwepo kwa makaburi 42 ya halaki katika eneo la Kasai tangu Agosti 2016.
Hapo Machi 8, 2017, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein, ametoa wito wa kuundwa tume maalamu ya uchunguzi juu ya vurugu zinazofanyika katika sehemu ya Kasai. Lakini wakati huo maafisa kutoka Congo waliahidi kufanya upepelezi wao, na Machi 22, walikubali kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Africa. Lakini uchunguzi huo haujasonga mbele na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hadi sasa hawajaweza kushirikiana na wachunguzi wa Congo, lilisema shirika hilo.
Aprili 9, Kamishna mkuu huyo alisema kuwa kuna ukosefu wa hatua muhimu kutoka serikali ya Congo za kuhakikisha kuwa uchunguzaji huo utakuwa wa haraka, wa wazi na huru.
Mgogoro wa Kasai unahusu utawala wa sehemu hiyo na nani kuwa kiuongozi, lakini bila ya shaka siasa za taifa zinahusika ambapo jeshi la Congo linawaunga mkono wale wanaomuunga mkono rais Joseph Kabila na muungano wake wa kisiasa, na baadhi ya wanachama wa vikundi vya KAMUINA NSAPU wako karibu na upinzani.
Vurugu zilianza kupamba moto Kasai, pale kikosi cha ndani cha usalama kilipomuuwa KAMUINA NSAPU ambaye ndiye mrithi wa utawala katika kijiji cha Tshimbulun hapo August 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la haki za binadamu Paul Nsapu amesema kuwabaraza la haki za binadamu lazima lijihusishe katika kuwasaidia na kuwalinda raia na lazima litilie mkazo katika kutafuta haki, na wale waliohusika katika vurugu hilo na unyaunyasaji kutoka pande zote mbili lazima wachukuliwe hatua.
Mwandishi: Najma Said/HRW/press Human Rights Watch Press
Mhariri : Josephat Charo