1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji ya kisiasa yaongezeka Burundi

2 Mei 2012

Ripoti ya Shirika la haki za binaadamu-Human Righjts Watch-inasema tangu mwishoni mwa mwaka 2010 kumefanyika mlolongo wa mauaji katika mashambulizi ya kisiasa nchini Burundi.

https://p.dw.com/p/14nvd
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre NkurunzizaPicha: AP

Mauaji hayo baadhi yamefanywa na vyombo vya usalama, wanachama wa chama tawala na pia makundi ya upinzani yenye silaha, na hivyo kuashiria jinsi dola inavyoshindwa kuwalinda raia wake.

Ripoti hiyo yenye kurasa 81 iliyopewa jina "Ukiwa hai hauwezi kuwa na amani, kuongezeka kwa ghasia za kisiasa ndani ya Burundi." Inabainisha kuwa mauaji haya ni ya kulipiza kisasi hasa yaliyofanywa na chama cha siasa cha CNDD-FDD dhidi ya chama cha FNL huku haki ya kutopatikana kwa familia za waanga wa mauaji hayo.

Ripoti hii imeonyesha namna serikali ya Burundi ilivyokusudia kubana uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya kijamii vinayopinga mauaji hayo.

Chama tawala kilikuwa na nafasi ya kuanza ukurasa mpya kwa Burundi baada ya uchaguzi wa 2010, anasema Mkurugenzi wa Humani Right Watch kwa Bara la Afrika Daniel Bekeke. Badala yake kumeshuhudiwa vitendo vya kupangilia vya kuwaandama wapiganaji wa zamani na wanachama wa vyama vya kisiasa vya upinzani-wengi wakiwa wale waliokataa kusalimu amri na kufuata shinikizo la kuwataka wajiunge na chama tawala CNDD-FDD.

Esther Kamatari ambaye alionyesha nia ya kugombea Urais mwaka 2004
Esther Kamatari ambaye alionyesha nia ya kugombea Urais mwaka 2004Picha: AP

Shirika hilo limezitaka pande zote mbili, serikali na makundi ya upinzani, kulaani mauaji yaliofanywa na wanachama wao na kuchukuwa hatua ya kuzuwia ghasia zaidi. Pia serikali imetakiwa kuepusha mauaji na vitisho vya mauaji dhidi ya wanachama wa zamani wa makundi ya upinzani, yanayofanywa na idara za usalama na kundi la vijana wa CNDD-FDD wanaojulikana kama IMBONERAKURE.

Taarifa hii inatokana na utafiti wa kina tangu mapema 2011 hadi 2012 kwa kuzungumza na waanga, ndugu wa waanga na mashahidi huku ikijuimuisha mauaji ya watu 37 katika klabu moja katika mji wa Gatumba septemba mwaka 2012.

Mauaji ya Audace Vianney Habonarugira kutoka chama cha FNL ambaye aliuwawa Julai 2011 ambaye alikuwa akisakwa mno na Polisi, Jeshi na idara ya usalama baada ya kutoa ushahidi wake kwa Shirika hilo la Human Right Watch.

Huku mauaji ya Pascal Ngendakumana na Albert Ntiranyibangira pamoja binti mdogo waliokuwa nae jirani waliuwawa na watu wanaodhaniwa ni wanachama wa FNL ambapo haya yalikuwa ni mauaji kwa wanasiasa wa kawaida kufanywa na chama kingine cha siasa.

Mauaji ya Gatumba yatokea

Mapema 2011 Serikali ya Burundi ilipunguza mauaji hayo kwa kujidai kuwa mauaji hayo yanafanywa na waalifu kama walivyo waalifu wengine lakini julai hali ikawa mbaya mno na Septemba ndipo mauaji ya Gatumba yakafanyika bila ya kufanyika lolote huku wauaji wakibaki mitaani na wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Katika kesi moja jaji hakutokea kabisa mahakamani pamoja na baadhi ya maafisa wakubwa wa polisi. Jaji akatoa hukumu katika muda mfupi tu, bila ya wahanga kutendewa haki.

Katika mauaji ya Gatumba serikali ya Burundi ilisema bayana ingefanya uchunguzi lakini hakukuwa na lolote lile lililofanyika na hayo kuthibitishwa na ndugu wa jamaa wa wahanga hao.

Hali hii imesababisha kutokuwapo na imani na vyombo vya usalama na serikali kwa kushindwa kuwa wakweli kuhusiana na mauaji haya.

Vyombo vya habari vyakumbwa na janga hili

Waandishi wa habari nao wamekumbwa na janga hilo. Kwa mfano Bob Rugurika ambaye alikuwa mhariri wa Redio Moja binafsi RPA aliitwa kuhojiwa na mwendesha mashitaka mara zaidi ya nane kati ya julai na novemba 2011 juu ya vipindi vya Redio hiyo ikituhumiwa kwa kuripoti mauaji hayo.

Hiyo ni Aprili 27, 2003 ambapo mtoto mdogo akiangalia mabaki ya nyumba yao baada ya kushambuliwa kwa bomu
Hiyo ni Aprili 27, 2003 ambapo mtoto mdogo akiangalia mabaki ya nyumba yao baada ya kushambuliwa kwa bomuPicha: AP

Pierre Claver Mbonimpa ambaye ni rais wa chama cha haki za binadamu ambaye aliikosoa waziwazi serikali hiyo juu ya mpango wa kuwamaliza wapinzani aliandikiwa barua na Waziri wa mambo ya ndani akitakiwa ajieleze kutoa taarifa zisizo sahihi kwa umma.

Shirika hilo la Human Rights Watch linadokeza kwamba hali ya usalama mwaka huu 2012 kidogo ni afueni, na mauaji ya kisiasa yamepungua.

Mwandishi:Adeladius Makwega/HRW Report

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman