Mawaziri wa NATO wakutana Brussels kujadili usalama
3 Desemba 2024Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atashiriki mkutano huo ambao huenda ukawa wa mwisho wa ngazi za juu kushiriki, kabla utawala wa rais Joe Biden kuondoka madarakani.
Miongoni mwa ajenda za mwanzo kwenye mkutano huo ni suala la kuimarisha uungaji mkono kwa Ukraine kabla ya kurudi Donald Trump madarakani Januari mwakani.
Rais Zelensky aitaka Marekani iushawishi Umoja wa Ulaya ukubali kuikaribisha Ukraine NATO
Masuala ya kipaumbele katika ushirikiano wa kiusalama kati ya Marekani na Ulaya yatajadiliwa ikiwemo kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi, lakini pia kuimarisha ushirikiano na washirika wa NATO wa kusini katika kanda ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, na Sahel. Mkutano huo pia utajadili maandalizi ya mkutano ujao wa kilele utakaofanyika The Hague mwezi Juni.