Mawaziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini na Kusini wakutana
27 Novemba 2007Matangazo
PYONGYANG. Mawaziri wa Ulinzi wa Korea Kusini na Kaskazini wameanza mazungumzo yao katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang yenye kulenga kupunguza uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Wanatarajiwa pia kujadili maeneo ya pamoja katika uvuaji wa samaki na kuhitimisha vita kati yao juu ya haki za uvuvi katika eneo la bahari.
Huo ni mkutano wa kwanza kati ya mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili katika kipindi cha miaka saba iliyopita na wa pili katika kipindi cha miaka 50.
Mazungumzo hayo yanafuatia mkutano wa mwezi uliyopita kati ya Rais Kim Jong il wa Korea Kaskazini na mwenziye Roo Moo-hyun wa Korea Kusini.