Mazungumzo kati ya M23 na serikali bado yanaendelea
11 Desemba 2012Matangazo
Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka DRC ukiongozwa na Mufti wa waislamu wa Kongo akiwa pia mwenyekiti wa muungano wa madhebu ya Congo kwa ajili ya amani Sheikh Abdallah Mangala Luaba, ulikutana kwa mazungumzo na kiongozi wa madhehebu ya Uganda kwa uwepo wa wajumbe wa mashirika ya kiraia wa nchi zote mbili, kujadili hali ya usalama mashariki mwa DRC.
John Kanyunyu alizungumza na Sheikh Abdallah Mangala, ambaye anatuambia kwanini walikutana.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: John Kanyunyu
Mhariri: Saumu Yusuf