1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kati ya PNU ya Kibaki na ODM ya Odinga yaanza rasmi Kenya

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzMO

NAIROBI:

Kuna matumaini kuwa masuala ya mda mfupi yanaweza yakatatuliwa katika kipindi cha wiki 4.Hayo ameyasema leo katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan akifungua mazunguzo ya mani mjini Nairobi.Juhudi za Annan zinafuata ghasia ambazo watu kadhaa wameuliwa.Na mwanasiasa wa upinzani nae amekuwa mhanga wa ghasia za kikabila zinazoendelea nchini humo.Polisi inasema kuwa mbunge wa chama cha Orange Democratic Movement-ODM- Mugabe Were, alipigwa risasi mbili kichwani mara punde tu alipowasili nyumbani kwake mjini Nairobi.Mda mchache baadae magenge ya watu yalianza kupigana katika mtaa wa mabanda wa Kibera,karibu na mahali pa tukio.Polisi inasema mauaji yalikuwa ni tukio la kihalifu,hata hivyo yeye Raila Odinga amekataa kauli ya polisi akisema mauaji ya mbunge wa chama chake ni ya kisiasa.Ghasia pia zimekuwa zikiongezeka katika miji ya Naivasha na Nakuru inayopatikana katika mkoa wa Bonde la Ufa.Ndege za helikopta za kijeshi zimelazimika kufyatulia risasi genge moja ambalo lilikuwa linajaribu kushambulia kundi la kabila lingine.Msemaji wa Bw Odinga –Salim Lone asema ikiwa hatua muafaka hazitachukuliwa ghasia zinaweza kuongezeka.

Watu zaidi ya 800 wameuawa na wengine karibu robo millioni wameachwa bila ya makazi tangu uchaguzi wa mwezi jana ambao upande wa upinzani unadai kulikuwa na uibiaji. Kwa mda huohuo mazungumzo kati ya wafuasi wa chama cha ODM cha Raila Odinga na wa rais Mwai Kibaki yalipangwa kuanza mjini Nairobi.