1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sri Lanka na waasi wa Tamil yafunguliwa mjini Geneva

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyM

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sri Lanka na waasi wa Tamil yameanza kwa mara ya kwanza mjini Geneva hii leo baada ya kupita karibu miezi minane.Mpatanishi wa kutoka Norway,Erik Solheim amezitolea mwito pande zinazohasimiana zionyeshe moyo wa maridhiano.Wananchi wa Sri Lanka na jumuia ya kimataifa wamechaanza kupotelewa na subira-amesema bwana Erik Solheim. Norway ilifanikiwa miaka minne iliyopita kuzitanabahisha pande hizo mbili zitiliane saini makubaliano ya kuweka chini silaha.Licha ya makubaliano hayo lakini,maapigano yamekua yakiendelea Sri Lanka tangu miezi kumi iliyopita na kugharimu maisha ya watu wasiopungua elfu tatu.Hatua za usalama zimeimarishwa hii leo nchini humo baada ya askari polisi sita kujeruhiwa katika shambulio hivi karibuni.