Miongoni mwa ripoti za Afrika wiki hii ni pamoja na kurejea nyumbani Kongo aliyekuwa kiongozi wa waasi wa UPC Thomas Lubanga. Nchini Tanzania kampeini za uchaguzi zashika kasi visiwani Zanzibar mgombea urais wa upinzani Maalim Seif Sharif Hamadi awekewa pingamizi na nchini Mali jeshi lililotwaa madarakani lazidi kushinikizwa likabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia. Ungana na Saumu Mwasimba