1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za hatua ya 16 zapangwa mjini Nyon

15 Desemba 2014

Mabingwa watetezi Real Madrid watakuana na Schalke 04, Barcelona watashuka dimbani na Manchester City na Chelsea watamenyana na Paris Saint Germain katika mechi tatu ambazo ni marudio ya msimu uliopita.

https://p.dw.com/p/1E4Md
UEFA Champions League Logo

Real MADRID iliibumburusha Schalke kutoka duru ya 16 za mwisho kwa kuwafunga jumla magoli 9 – 2, wakati Barcelona wakipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Manchester City nao Chelsea wakawapiga PSG kwa sheria ya magoli ya ugenini katika robo fainali.

Borussia Dortmund iliibwaga Juventus magoli matatu kwa moja katika fainali ya mwaka wa 1997, na timu hizo mbili zimepangwa kupambana tena. Makamu bingwa wa msimu uliopita Atletico Madrid watakutana na Bayer Leverkzsen katika mchuano mwingine kati ya Uhispania na Ujerumani.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atamenyana na klabu yake ya zamani AS Monaco, katikamchuano wa ushindani kwa mara ya kwanta wakati washindi mara tano Bayern Munich wakipangwa kupambana na Shakhtar Donetsk. Klabu ya Uswisi Basel ikashuka dimbani na Porto ya Ureno.

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Februari 17/18 na Feb 24/28 wakati za mkondo wa pili zikichezwa mnamo Machi 10/11 na Machi 17/18 mwaka ujao. Fainali itakuwa mjini Berlin Juni 6.

Na katika dimba la Europa League, bingwa mtetezi Sevilla atachuana na Borussia Moenchengladbach katika hatua ya 32 za mwisho. Celtic imepangwa kupambana na Inter Milan. Pia mabingwa mara tano wa Ulaya Liverpool watachuana na Besiktas, Tottenham itachuana na Fiorentina na Napoli itacheza na Trabzonspor.

Katika mechi nyingine, Roma itakuana na Feyenoord, Ajayx dhidi ya Legia Warsaw na Everton itampambana na Young boys. Huku UEFA ikizitenganisha timu za Urusi na Ukraine kwa sababu za kisiasa, Zenit St Petersburg imepangwa na PSV Eindhoven. Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Februari 19 na ya marudio zikichezwa Februari 28.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu