Merz awasili Ukraine kwa mazungumzo
9 Desemba 2024Matangazo
Merz amesema baada ya kuwasili mjini Kyiv kuwa anataka kuihakikishia Ukraine kuwa chama chake cha kihafidhina kinaiunga mkono.
Amesisitiza kuwa vita vya Ukraine havina budi kumalizika na amani inapaswa kurejeshwa barani Ulaya.
Kiongozi huyo wa CDU amekuwa akionesha upinzani zaidi dhidi ya Urusi kuliko Kansela Olaf Scholz akisema kuwa Ujerumani inapaswa kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Taurus.
Ukraine imekuwa ikiyasubiri makombora hayo kwa muda mrefu ili kuyatumia kama Kremlin haitoacha kuishambulia miundombinu yake ya kiraia.