Nchi tofauti zina mifumo tofauti ya afya na bila shaka kila mmoja anauelewa vyema mfumo wa afya wa nchi yake, ila masuala tofauti aghalabu yakiwa ya kazi, yanaweza kukufanya ukasafiri na kulazimika kuishi katika nchi ya kigeni. Andamana na Jacob Safari katika Sura ya Ujerumani ufahamu jinsi mfumo wa afya nchini Ujerumani ulivyo.