mgomo wa wachimba mkigodi ya dhahabu unaendelea kwa siku ya tatu hii leo nchini Afrika kusini
9 Agosti 2005Mgomo wa wachimba migodi ya dhahabu nchini Afrika kusini unaendelea kwa siku ya tatu hii leo.Chama kinachopigania masilahi ya wafanyakazi kimelikataa pendekezo la kampuni la ANGLOGOLD la kuongeza kwa asili mia 6.5 kiwango cha mishahara ya wafanyakazi.Duru za chama hicho kinachopigania masilahi ya wafanyakazi zinasema mazungumzo pamoja na kampuni la ANGLOGOLD hayakusaidia kitu.Waajiriwa wanadai nyongeza ya mishahara kati ya asili mia 8 na asili mia 12.Wachimba migodi wengine elfu kumi wamejiunga na mgomo huo.Kwasasa wachimba migodi laki moja na elfu kumi kati ya laki moja na 30 elfu wamejiounga na mgomo huo.Wachimba migodi wameacha kazi tangu jumapili iliyopita baada ya mazungumzo ya nyongeza ya mishahara kutoleta tija wiki iliyopita.Hii ni mara ya kwanza kwa kiwanda cha dhahabu kukabwa na mgomo nchini Afrika kusini tangu miaka 18 iliyopita.