Wakimbizi katika mji wa Beni ulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanalalamika kuwa watoto wao wanabaguliwa na viongozi wa baadhi ya shule mjini humo, wakati tayari muhula wa kwanza wa mwaka wa masomo ukiwa umeanza Jumatatu wiki hii. Wanasema hali hiyo haielweki wakati sera ya serikali ikiwa ni elimu ya msingi kwa watoto wote, tena bila malipo.