1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Miaka 25 ya Rais Putin: Kwanza rafiki, na sasa adui

31 Desemba 2024

Mkesha wa mwaka mpya wa 1999 aliuanza kama mwanamageuzi na kubadilika kuwa mbabe wa kivita. Uhusiano wa EU, NATO na Urusi ya Putin umebadilikaje?

https://p.dw.com/p/4oi6k
Russia | Putin na Yeltsin 1999
Agosti 10, 1999: Rais wa Urusi Boris Yeltsin (kulia) akitabasamu wakati wa kikao cha kaimu Waziri Mkuu Vladmir Putin katika Ikulu ya Kremlim.Picha: ITAR-TASS/dpa/picture alliance

Mnamo Agosti 1999, Vladimir Putin aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Shirikisho la Urusi, na mwishoni mwa mwaka huo, alichukua nafasi ya Rais Boris Yelzin aliyekuwa mgonjwa.

Katika hotuba yake ya mwanzo, Putin alisisitiza kuwa Urusi ilikuwa na itaendelea kuwa taifa lenye nguvu kubwa. Barani Ulaya, alionekana kama mrekebishaji aliyekuja kuirekebisha Urusi iliyokuwa imevurugika katika miaka ya tisini.

Mwaka 2001, Rais wa Marekani George W. Bush alimwita Putin "mwaminifu na muwazi" baada ya mkutano wao wa kilele. Putin pia alitoa pendekezo la ushirikiano wa usalama kati ya Urusi na Ulaya katika hotuba yake kwa Bunge la Ujerumani.

Ushirikiano wa kimkakati kati ya EU na Urusi ulianza, huku NATO ikifungua ofisi mjini Moscow na Urusi ikiweka uwakilishi wake Brussels.

Ujerumani Heiligendamm | Mkutano wa Kilele wa G8 2007
Putin (wa nne kutoka kulia), akiwa na viongozi wa mataifa ya kundi la G8 - kutoka kushoto; Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Marekani George Bush, Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair, Rais wa Italia Romano Prodi na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Jose Manquel Barroso, Juni 7, 2007.Picha: AP

Mabadiliko ya Putin

Mwaka 2006, katika mkutano wa usalama wa Munich, Putin alianzisha mabadiliko ya sera, akilalamika kuwa Magharibi haikuitambua Urusi kama taifa lenye nguvu.

Alikosoa upanuzi wa NATO na kudai kuwa ahadi za kutojitanua kwa jumuiya hiyo ya kijeshi karibu na mipaka ya Urusi zilipuuzwa. Hata hivyo, Urusi ilikuwa imekubali upanuzi huo katika makubaliano ya mwaka 1997.

Soma pia: Putin aweka rekodi kwenye matokeo ya uchaguzi Urusi

Mwaka 2008, Putin alionyesha nguvu zake za kijeshi kwa kuingilia mgogoro nchini Georgia na kuyaleta maeneo ya Abkhazia na Ossetia Kusini chini ya udhibiti wa Urusi.

Vita vya Putin

Mwaka 2014, baada ya mapinduzi ya Maidan nchini Ukraine yaliyomuondoa Rais aliyekuwa rafiki wa Urusi, Putin alianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Aliitwaa kwa nguvu rasi ya Crimea na kuwasaidia wanamgambo wa Urusi katika sehemu za mashariki mwa Ukraine.

Mtaifa ya magharibi yalijibu kwa vikwazo na juhudi za upatanishi, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Minsk, ambao haukuwahi kufanikisha amani ya kudumu.

Valery Gerasimov na Putin - Mapitio ya vita vya Ukraine
Putin Mkuu wake wa Jeshi Valery Gerasimov wakihudhuria mkutano wa bodi ya wizara ya ulinzi kujadili vita vya Ukraine.Picha: POOL/Grigiry Sysoyev/AFP/Getty Images

Mahusiano kati ya Urusi na mataifa ya magharibiyalizorota zaidi, huku Putin akionekana zaidi kama mtawala wa kiimla.

Soma pia: Putin awaonya Scholz na Macron dhidi ya kuipa silaha Ukraine

Kufikia mwaka 2022, baada ya Urusi kushambulia Ukraine kwa kiwango kikubwa, NATO ilimtaja Putin kama "tishio kubwa zaidi kwa amani barani Ulaya."

Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo vikubwa dhidi ya Urusi na kuanza juhudi za kujiondoa kwenye utegemezi wa nishati ya Urusi, ingawa bado unaendelea kuitegemea nishati hiyo kwa kiasi.

Miaka 25 ya Putin Madarakani

Miaka 25 tangu Putin alivyoingia madarakani, NATO sasa inajiandaa kwa mashindano mapya ya kijeshi dhidi ya Urusi. Kuzuia uchokozi wa Urusi imekuwa jukumu kuu la muungano huo.

Putin aapishwa kuongoza muhula wa nne

Licha ya vikwazo na kushuka kwa biashara na Urusi, baadhi ya sekta kama vyakula, dawa, na kemikali hazijaathiriwa, na biashara ya Urusi na Ulaya inaendelea, ingawa kwa kiwango kidogo.

Urithi wa Putin unaendelea kuwa wa mabishano makubwa, ukionyesha mabadiliko makubwa ya mahusiano ya kimataifa na usalama barani Ulaya.