1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo ya Olimpiki yaanza jijini London

28 Julai 2012

Baada ya ngoja ngoja ya muda mrefu hatimaye mchezo ya Olimpiki ya London 2012 imefunguliwa rasmi katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Olimpiki jijini London, Uingereza.

https://p.dw.com/p/15fnI
The Olympic cauldron is lit during the Opening Ceremony at the 2012 Summer Olympics, Saturday, July 28, 2012, in London. (AP Photo/Mark Baker)
Eröffnungsfeier Olympiade London 2012Picha: dapd

Kulikuwa na mbwembwe za kila aina huku muigizaji filamu aliyejifanya kuwa Malkia Elizabeth, akitumia mwamvuli kuruka na kutua uwanjani akiwa na James Bond. Wakati wakitua uwanjani, kwaya ya watoto ilitanda angani kumwonyesha heshima Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 86, kwa wimbo “God Save the Queen”. Kisha kukawa na matukio kuonyesha Wasanii na Sanaa ya Uingereza, kuwakumbuka watu kama Peter Pan, Harry Potter, Mary Poppins, Chariots of Fire na wengine wengi.

Burudani lilianza kwa ndege za kviita kupaa angani zikitoa moshi wa rangi nyekundu, nyeuoe na samawati juu ya uwanja uliofurika mashabiki 80,000, na kuanzisha tamasha hilo lililojaa watu mashuhuri, waigizaji filamu, na hata wanamichezo maarufu.

Gwaride la wanariadha katika hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki
Gwaride la wanariadha katika hafla ya ufunguzi wa michezo ya OlimpikiPicha: Reuters

Na kukamilisha uhondo huo wa saa tatu ulioandaliwa na mmoja wa wanafilamu mashuhuri wa Uingereza, mshindi wa tuzo ya Oscar, Danny Boyle, wakaazi wa London walishuhudia mripuko wa fataki na kuungana katika kuimba wimbo na mwanamuziki Paul McCartney.

Wapeperusha bendera

Gwaride la mataifa yanayoshiriki liliwajumuisha takribani wanariadha 10,500 wanaoshiriki katika michezo hiyo, huku kukiwa na bendera 204 za kitaifa zilizopeperushwa angani. Ugiriki ilichukua uongozi na Timu ya Uingereza ikashika nafasi ya mwisho kama mwenyeji. Gwaride la wanariadha ni utamaduni ulioanza katika michezo ya kwanza ya Olimpiki ya London mwaka wa 1908.

Hotuba za waandalizi wa Olimpiki zilifuata na hotuba ya Malkia akifungua rasmi michezo hiyo. Hii kisha ikatoa nafasi ya kubeba bendera ya Olimpiki na wageni maalum, kama vile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, na wanamichezo mashuhuri kama vile mwaandondi Muhammad Ali, hadi kwenye mlingoti wa bendera. Halafu ikapandishwa kwa shangwe na vigelegele.

Mwenge wa Olimpiki kuwaka hadi siku ya mwisho ya michezo
Mwenge wa Olimpiki kuwaka hadi siku ya mwisho ya michezoPicha: dapd

Kiapo cha olimpiki kikachukuliwa na Sarah Stevenson, mshindani katika mchezo wa TaeKwonDo, kwa niaba ya wanariadha. Eric Farell, kocha wa mchezo wa kuendesha mtumbwi, akala kiapo wka niba ya makocha.

Wakati huo huo, boti iliyokuwa na mwanasoka David Beckham iliwasili uwanjani, na kumkabidhi mwenge wa Olimpiki Steven Redgrave, ambaye kisha alikwenda katika uwanja wa Olimpiki.

Kisha vijirungu vidogo vikawashwa na wanariadha saba chipukizi, wakiwakilisha matumaini ya Uingereza katika maisha ya usoni. Maelezo kuhusu wale watakaobeba mwenge kwa mara ya mwisho yalikuwa yamefichwa. Baada ya kuwashwa, mienge hiyo ilipandishwa kwa uzuri ili kutengeneza mwenge wa Olimpiki. Fataki zilifyatuliwa huku mwanamuziki Sir Paul McCartney akimalizia sherehe hizo kwa kuuongoza umati.

Mwandishi: Bruce Amani/AP/Reuters

Mhariri: Mohamed Khelef