Michuano ya Champions League yarejea
5 Machi 2018Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Porto mwezi uliopita uliihakikishia Liverpool nafasi katika robo fainali lakini kocha wa Liverpool Juergen Klopp amesema atateua kikosi imara kwa mchezo huo licha ya kuelekea Manchester United mwishoni mwa juma. Watapambana , ndicho watakachokifanya. Ni Wareno na wanajihisi fahari na watataka kupambana. Wanataka kulipiza kisasi. Amesema Klopp kuhusiana na mchezo wa kesho. Lakini pambano linalosubiriwa kwa hamu hapo kesho ni baina ya Paris Saint Germain na Real Madrid. Baada ya ushindi mnono wa mabao 3-1 wa Real Madrid dhidi ya PSG katika mchezo wa kwanza, mchezo huo una viashiria vyote kwamba moto utawaka wakati PSG ikitaka kuonesha kwamba wanaweza na wako tayari kulinyakua kombe hilo.
Lakini kikosi cha PSG kitamkosa kiungo nyota mchezeshaji Neymar ambaye aliondolewa kutoka hospitali jana Jumapili kwa helikopta , siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji , na kuanza hatua za kupona kabla ya kurejea na kujiunga na kikosi cha Brazil katika kombe la dunia mwaka huu. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 kiungo mchezeshaji wa Paris Saint Germain alipelekwa katika uwanja wa ndege wa Belo Horizonte kwa helikopta, ambako alikotarajiwa kwenda katika nyumba yake ya kifahari katika mji wa kitalii wa Mangaratiba kiasi ya kilometa 100 kutoka mjini Rio de Janeiro.
Jumatano itakuwa zamu ya Tottenham Hot Spurs ikiikaribisha Juventus Turin na Manchester City itakwaana na Basel ya Uswisi.
Urusi inawanyamazisha wenye viwanda vikubwa ambao wana hofu na kuonekana kuvifunga viwanda kadhaa vikubwa kuepusha ajali na kitisho cha mashambulizi ya kigaidi wakati wa mashindano ya kombe la dunia mwaka huu. Kusitisha uzalishaji kunaelekea ni hatua ambayo Urusi inataka kuichukua ikiwa ni inayoonekana kuwa Urusi iko tayari kupoteza mapato wakati itakapokuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya kandanda kwa mara ya kwanza nchini humo kuanzia Juni 14.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu