Michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika, itaanza leo nchini Misri. Kwa mara ya kwanza timu 24 zitashiriki michuano hiyo. Mechi ya ufunguzi ni kati ya wenyeji Misri dhidi ya Zimbabwe. nchi nne za Afrika mashariki zinashiriki nazo ni Kenya, Tanzania, Uganda na Burundi.